Jeremiah 34:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: Nenda ukaongee na Sedekia, mfalme wa Yuda. Mwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nimeutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Enenda ukaseme na Sedekia, mfalme wa Yuda, ukamwambie, Bwana asema hivi, Tazama, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: Nenda ukaongee na Sedekia, mfalme wa Yuda. Mwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nimeutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli, kusema: Nenda kwa Sedekia, mfalme wa Yuda na umwambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Israeli, kusema: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nenda ukaseme na Sedekia, mfalme wa Yuda, ukamwambie, BWANA asema hivi, Tazama, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: Nenda ukaongee na Sedekia, mfalme wa Yuda. Mwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nimeutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Nenda kumwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, ukimwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utaniona, nikiutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli, auteketeze kwa moto!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Enenda ukaseme na Sedekia, mfalme wa Yuda, ukamwambie, BWANA asema hivi, Tazama, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kwenda usemezane na Zedekia, mufalme wa Yuda. Umwambie kwamba mimi Yawe ninasema hivi: Nimeutia muji huu katika mikono ya mufalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto.