Jeremiah 34:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watatiwa mikononi mwa maadui zao, na mikononi mwa watu wanaotaka kuwaua. Maiti zao zitaliwa na ndege wa angani na wanyama wa porini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nitawatia mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao. Maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege za mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watatiwa mikononi mwa maadui zao, na mikononi mwa watu wanaotaka kuwaua. Maiti zao zitaliwa na ndege wa angani na wanyama wa porini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nitawatia mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao. Maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nitawatia mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao. Maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege wa mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watatiwa mikononi mwa maadui zao, na mikononi mwa watu wanaotaka kuwaua. Maiti zao zitaliwa na ndege wa angani na wanyama wa porini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hao wote nitawatia mikononi mwa adui zao namo mikononi mwao wanaozitafuta roho zao, nayo mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na cha nyama wa porini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege za mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watatiwa katika mikono ya waadui zao, na katika mikono ya watu wanaotaka kuwaua. Maiti zao zitakuliwa na ndege na nyama wa pori.