Jeremiah 34:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nitawaamuru nao wataurudia mji huu. Wataushambulia, watauteka na kuuteketeza kwa moto. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa bila wakazi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitatoa amri, asema Mwenyezi Mungu, nami nitawarudisha tena katika mji huu. Watapigana dhidi yake, wautwae na kuuteketeza kwa moto. Nami nitaiangamiza miji ya Yuda ili pasiwe na yeyote atakayeweza kuishi humo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, nitawapa amri yangu, asema Bwana, na kuwarejeza kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nitawaamuru nao wataurudia mji huu. Wataushambulia, watauteka na kuuteketeza kwa moto. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa bila wakazi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitatoa amri, asema BWANA, nami nitawarudisha tena katika mji huu. Watapigana dhidi yake, watautwaa na kuuteketeza kwa moto. Nami nitaiangamiza miji ya Yuda hivyo pasiwe na ye yote atakayeweza kuishi humo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitatoa amri, asema bwana, nami nitawarudisha tena katika mji huu. Watapigana dhidi yake, wautwae na kuuteketeza kwa moto. Nami nitaiangamiza miji ya Yuda hivyo pasiwe na yeyote atakayeweza kuishi humo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejesha kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nitawaamuru nao wataurudia mji huu. Wataushambulia, watauteka na kuuteketeza kwa moto. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa bila wakazi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona nikiwaagiza na kuwarudisha penye mji huu, waupigie vita, wauteke, wauteketeze kwa moto; nayo miji ya Yuda nitaitoa kuwa mapori tu, pasikae mtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejeza kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaamuru nao wataurudia katika muji huu. Wataushambulia, watauteka na kuuteketeza kwa moto. Nitaifanya miji ya inchi ya Yuda kuwa ukiwa bila wakaaji. –Ni ujumbe wa Yawe.