Jeremiah 34:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawe hutatoroka mikononi mwake, bali kwa hakika utatekwa na kupelekwa kwake; utaonana na mfalme wa Babuloni macho kwa macho, na kuongea naye ana kwa ana; kisha, utakwenda Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hutaweza kuepuka mkono wake, bali hakika utatekwa na kukabidhiwa kwake. Utamwona mfalme wa Babeli kwa macho yako mwenyewe, naye atazungumza nawe ana kwa ana. Nawe utaenda Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena wewe hutaokoka mkononi mwake, lakini utakamatwa kweli kweli, na kutiwa katika mikono yake; na macho yako yatayatazama macho ya mfalme wa Babeli, naye atasema nawe mdomo kwa mdomo, nawe utakwenda Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawe hutatoroka mikononi mwake, bali kwa hakika utatekwa na kupelekwa kwake; utaonana na mfalme wa Babuloni macho kwa macho, na kuongea naye ana kwa ana; kisha, utakwenda Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hutaweza kuepuka mkono wake bali hakika utatekwa na kukabidhiwa kwake. Utamwona mfalme wa Babeli kwa macho yako mwenyewe naye atazungumza nawe ana kwa ana. Nawe utakwenda Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hutaweza kuepuka mkono wake, bali hakika utatekwa na kukabidhiwa kwake. Utamwona mfalme wa Babeli kwa macho yako mwenyewe, naye atazungumza nawe ana kwa ana. Nawe utakwenda Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena wewe hutaokoka mkononi mwake, lakini hakika utakamatwa, na kutiwa katika mikono yake; na utatazamana macho kwa macho na mfalme wa Babeli, naye atasema nawe mdomo kwa mdomo, nawe utakwenda Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawe hutatoroka mikononi mwake, bali kwa hakika utatekwa na kupelekwa kwake; utaonana na mfalme wa Babuloni macho kwa macho, na kuongea naye ana kwa ana; kisha, utakwenda Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe hutaopoka mkononi mwake, kwani utakamatwa, utiwe mkononi mwake, nawe utaonana na mfalme wa Babeli macho kwa macho, atasema na wewe kinywa kwa kinywa, nawe utakwenda Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena wewe hutaokoka mkononi mwake, lakini utakamatwa kweli kweli, na kutiwa katika mikono yake; na macho yako yatayatazama macho ya mfalme wa Babeli, naye atasema nawe mdomo kwa mdomo, nawe utakwenda Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe hautatoroka toka mikono yake, lakini kwa hakika utatekwa na kupelekwa kwake; utaonana na mufalme wa Babeli macho kwa macho, na kusema naye kinywa kwa kinywa; kisha, utakwenda Babeli.