Jeremiah 34:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utakufa kwa amani. Na, kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika wazee wako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema, ‘Maskini! Mfalme wetu amefariki!’ Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bali utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee Mwenyezi Mungu!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
utakufa katika amani; na kwa mafukizo ya baba zako, wafalme wa zamani waliokutangulia, ndivyo watakavyokufukizia; nao watakulilia, Aa, Bwana! Kwa maana mimi nimelinena neno hili, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utakufa kwa amani. Na, kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika wazee wako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema, ‘Maskini! Mfalme wetu amefariki!’ Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee BWANA!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema BWANA.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee bwana!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema bwana.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
utakufa katika amani; na kama walivyofukizia baba zako, wafalme wa zamani waliokutangulia, ndivyo watakavyokufukizia; na kukulilia wakisema, Aa, BWANA! Kwa maana mimi nimelinena neno hili, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utakufa kwa amani. Na, kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika wazee wako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema, ‘Maskini! Mfalme wetu amefariki!’ Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utakufa na kutulia; kama baba zako waliokuwa wafalme wa kwanza, waliokuwa mbele yako, walivyowashiwa mioto, ndivyo, watakavyokuwashia nawe mioto wakikuombolezea kwamba: E Bwana! Kwani hili ndilo neno, nililolisema mimi; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
utakufa katika amani; na kwa mafukizo ya baba zako, wafalme wa zamani waliokutangulia, ndivyo watakavyokufukizia; nao watakulilia, Aa, BWANA! Kwa maana mimi nimelinena neno hili, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utakufa kwa amani. Na kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika babu zako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema: Masikini! Mufalme wetu amekufa! –Ni ujumbe wa Yawe.