Jeremiah 34:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
watumwa wao wa Kiebrania wa kiume na wa kike, ili mtu yeyote asimfanye Myahudi mwenzake mtumwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mmoja alipaswa kuwaacha huru watumwa wake Waebrania, wanawake na wanaume. Hakuna yeyote aliyeruhusiwa kumfanya Myahudi mwenzake kuwa mtumwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake, na kila mtu amweke huru mjakazi wake, ikiwa yule mwanamume au yule mwanamke ni Mwebrania; mtu ye yote asiwatumikishe, yaani, asimtumikishe Myahudi, nduguye;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
watumwa wao wa Kiebrania wa kiume na wa kike, ili mtu yeyote asimfanye Myahudi mwenzake mtumwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja alipaswa kuwaacha huru watumwa wake wa Kiebrania wanawake na wanaume, hakuna mtu ye yote aliyeruhusiwa kumshikilia Myahudi mwenzake kama mtumwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mmoja alipaswa kuwaacha huru watumwa wake wa Kiebrania, wanawake na wanaume. Hakuna yeyote aliyeruhusiwa kumshikilia Myahudi mwenzake kama mtumwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake, na kila mtu amweke huru mjakazi wake, ikiwa yule mwanamume au yule mwanamke ni Mwebrania; mtu yeyote asiwatumikishe, yaani, asimtumikishe Myahudi, nduguye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
watumwa wao wa Kiebrania wa kiume na wa kike, ili mtu yeyote asimfanye Myahudi mwenzake mtumwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kila mtu amwachilie mtumwa wake na kijakazi wake walio wa Kiebureo, akiwapa ruhusa, wajiendee tu, tena mtu asimtumikishe tena mwenziwe kazi za kutumwa katika nchi ya Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake, na kila mtu amweke huru mjakazi wake, ikiwa yule mwanamume au yule mwanamke ni Mwebrania; mtu ye yote asiwatumikishe, yaani, asimtumikishe Myahudi, nduguye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
watumwa na wajakazi wao wa Kiebrania, kusudi mutu yeyote asimufanye Muyuda mwenzake kuwa mutumwa.