Jeremiah 35:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu hivi: Je, nyinyi hamwezi kupokea mafundisho na kusikia maneno yangu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, aliye Mungu wa Israeli, asemalo: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na watu wa Yerusalemu, ‘Je, hamwezi kujifunza kutoka kwa wana wa Rekabu, na kuyatii maneno yangu?’ asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Enenda ukawaambie wana wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, Je! Hamtaki kupokea mafundisho, myasikilize maneno yangu? Asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu hivi: Je, nyinyi hamwezi kupokea mafundisho na kusikia maneno yangu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, aliye Mungu wa Israeli, asemalo: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na watu wa Yerusalemu, ‘Je, hamwezi kujifunza kutoka kwa wana wa Rekabu na kuyatii maneno yangu?’ asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, aliye Mungu wa Israeli, asemalo: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na watu wa Yerusalemu, ‘Je, hamwezi kujifunza kutoka kwa wana wa Rekabu, na kuyatii maneno yangu?’ asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nenda ukawaambie wana wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, Je! Hamtaki kupokea mafundisho, myasikilize maneno yangu? Asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu hivi: Je, nyinyi hamwezi kupokea mafundisho na kusikia maneno yangu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Nenda kuwaambia watu wa Yuda nao wakaao Yerusalemu: Je? Hamtaki kuonyeka, myasikie maneno yangu? Ndivyo, asemavyo Bwana:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Enenda ukawaambie wana wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, Je! Hamtaki kupokea mafundisho, myasikilize maneno yangu? Asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kwenda uwaambie watu wa inchi ya Yuda na wakaaji wa Yerusalema hivi: Ninyi hamuwezi kupokea mafundisho na kusikia maneno yangu? –Ni ujumbe wa Yawe!