Jeremiah 35:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ile amri ambayo Yonadabu mwana wa Rekabu, aliwapa wanawe, kwamba wasinywe divai, imefuatwa; nao hawanywi divai mpaka siku hii ya leo, maana wametii amri ya mzee wao. Lakini mimi niliongea nanyi tena na tena, nanyi hamkunisikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Yonadabu mwana wa Rekabu aliwaagiza wanawe wasinywe divai, na agizo hilo wamelishika. Hadi leo hawanywi divai, kwa sababu wanatii amri ya baba yao. Nimenena nanyi tena na tena, lakini hamkunitii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ile amri ambayo Yonadabu mwana wa Rekabu, aliwapa wanawe, kwamba wasinywe divai, imefuatwa; nao hawanywi divai mpaka siku hii ya leo, maana wametii amri ya mzee wao. Lakini mimi niliongea nanyi tena na tena, nanyi hamkunisikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Yonadabu mwana wa Rekabu aliwaagiza wanawe wasinywe divai na agizo hilo wamelishika mpaka leo hawanywi divai kwa sababu wanatii amri ya baba yao. Lakini nimenena nanyi tena na tena, lakini hamkunitii mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Yonadabu mwana wa Rekabu aliwaagiza wanawe wasinywe divai, na agizo hilo wamelishika mpaka leo hawanywi divai, kwa sababu wanatii amri ya baba yao. Lakini nimenena nanyi tena na tena, lakini hamkunitii mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana wanaitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ile amri ambayo Yonadabu mwana wa Rekabu, aliwapa wanawe, kwamba wasinywe divai, imefuatwa; nao hawanywi divai mpaka siku hii ya leo, maana wametii amri ya mzee wao. Lakini mimi niliongea nanyi tena na tena, nanyi hamkunisikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maneno yake Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaagiza wanawe, wasinywe mvinyo, yametimizwa nao: hawanywi mvinyo hata siku hii ya leo, kwani wamelisikia agizo la baba yao. Mimi nami nimesema nanyi pasipo kuchoka kila kulipokucha, lakini hamkunisikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ile amri ambayo Yonadabu mwana wa Rekabu aliwapa wana wake kwamba wasikunywe divai, imefuatwa; nao hawakunywi divai mpaka siku hii ya leo, maana wametii amri ya babu yao. Lakini mimi nilisema nanyi tena na tena, nanyi hamukunisikiliza.