Jeremiah 35:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwapelekea tena na tena watumishi wangu wote yaani manabii wawaambieni kila mmoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu, arekebishe matendo yake na kuacha kuifuata na kuitumikia miungu mingine. Na kwamba mkifanya hivyo mtakaa katika nchi niliyowapa nyinyi na wazee wenu. Lakini nyinyi hamkunitegea sikio wala hamkunisikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara kwa mara nimewatuma kwenu watumishi wangu wote, manabii wakisema, “Geukeni, kila mmoja aiache njia yake mbaya, na kutengeneza matendo yake. Msiifuate wala kuitumikia miungu mingine. Ndipo mtakapoishi katika nchi niliyowapa ninyi na baba zenu.” Lakini hamkujali wala kunisikiliza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pia naliwapeleka watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiamka mapema na kuwapeleka, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwapelekea tena na tena watumishi wangu wote yaani manabii wawaambieni kila mmoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu, arekebishe matendo yake na kuacha kuifuata na kuitumikia miungu mingine. Na kwamba mkifanya hivyo mtakaa katika nchi niliyowapa nyinyi na wazee wenu. Lakini nyinyi hamkunitegea sikio wala hamkunisikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena na tena nimewatuma watumishi wangu wote manabii kwenu. Wakasema, “Kila mmoja wenu ni lazima ageuke na kuacha njia zake mbaya na kuyatengeneza matendo yake, msifuate miungu mingine ili kuitumikia. Ndipo mtakapoishi katika nchi niliyowapa ninyi na baba zenu.” Lakini hamkujali wala kunisikiliza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena na tena nimewatuma watumishi wangu wote manabii kwenu. Wakasema, “Kila mmoja wenu ni lazima ageuke na kuacha njia zake mbaya, na kuyatengeneza matendo yake. Msifuate miungu mingine ili kuitumikia. Ndipo mtakapoishi katika nchi niliyowapa ninyi na baba zenu.” Lakini hamkujali wala kunisikiliza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pia niliwatuma watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiwatuma pasipo kukoma, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiifuate miungu mingine, ili kuitumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwapelekea tena na tena watumishi wangu wote yaani manabii wawaambieni kila mmoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu, arekebishe matendo yake na kuacha kuifuata na kuitumikia miungu mingine. Na kwamba mkifanya hivyo mtakaa katika nchi niliyowapa nyinyi na wazee wenu. Lakini nyinyi hamkunitegea sikio wala hamkunisikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikatuma kwenu watumishi wangu wote walio wafumbuaji pasipo kuchoka kila kulipokucha kwamba: Rudini kila mtu katika njia yake mbaya na kufanya matendo mema! Msifuate miungu mingine kuitumikia! Ndipo, mtakaporudi katika nchi, niliyowapa baba zenu! Lakini hamkuyatega masikio yenu, wala hamkunisikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pia naliwapeleka watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiamka mapema na kuwapeleka, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwapelekea tena na tena watumishi wangu wote, ni kusema manabii wawaambie kila mumoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu, abadilishe matendo yake na kuacha kuifuata na kuitumikia miungu mingine. Na kwamba mukifanya hivyo mutakaa katika inchi niliyowapa ninyi na babu zenu. Lakini ninyi hamukunitegea sikio wala hamukunisikiliza.