Jeremiah 35:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yeremia aliwaambia Warekabu hivi: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Nyinyi Warekabu mmetii amri ya mzee wenu, mkashika maagizo yake yote na kutenda kama alivyowaamuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yeremia akaiambia jamaa ya Warekabi, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: ‘Mmetii amri ya baba yenu Yonadabu, na mmefuata mafundisho yake yote na mmefanya kila kitu alichowaamuru.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yeremia aliwaambia Warekabu hivi: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Nyinyi Warekabu mmetii amri ya mzee wenu, mkashika maagizo yake yote na kutenda kama alivyowaamuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yeremia akaiambia jamaa ya Warekabi, “Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Mmetii amri ya baba yenu Yonadabu na mmefuata mafundisho yake yote na mmefanya kila kitu alichowaamuru.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yeremia akaiambia jamaa ya Warekabi, “Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Mmetii amri ya baba yenu Yonadabu, na mmefuata mafundisho yake yote na mmefanya kila kitu alichowaamuru.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yeremia aliwaambia Warekabu hivi: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Nyinyi Warekabu mmetii amri ya mzee wenu, mkashika maagizo yake yote na kutenda kama alivyowaamuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walio wa mlango wa Rekabu Yeremia akawaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Kwa kuwa mmelisikia agizo la baba yenu Yonadabu, mkayashika maagizo yake yote, mkayafanya yote, kama alivyowaagiza,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yeremia aliwaambia Warekabu hivi: Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Ninyi Warekabu mumetii amri ya babu yenu, mukashika kanuni zake zote na kutenda kama alivyowaamuru.