Jeremiah 35:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nenda nyumbani kwa Warekabu, ukaongee nao. Kisha, walete katika chumba kimojawapo cha nyumba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, uwape divai wanywe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nenda kwa jamaa ya Warekabi, uwaalike waje kwenye moja ya vyumba vya pembeni vya nyumba ya Mwenyezi Mungu, na uwape divai wanywe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa Bwana, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nenda nyumbani kwa Warekabu, ukaongee nao. Kisha, walete katika chumba kimojawapo cha nyumba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, uwape divai wanywe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nenda kwa jamaa ya Warekabi na uwaalike waje kwenye moja ya vyumba vya pembeni vya nyumba ya BWANA na uwape divai wanywe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nenda kwa jamaa ya Warekabi, uwaalike waje kwenye moja ya vyumba vya pembeni vya nyumba ya bwana, na uwape divai wanywe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa BWANA, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nenda nyumbani kwa Warekabu, ukaongee nao. Kisha, walete katika chumba kimojawapo cha nyumba yangu mimi Mwenyezi-Mungu, uwape divai wanywe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nenda nyumbani mwao Warekabu kusema nao, uwapeleke Nyumbani mwa Bwana katika ukumbi mmoja, uwape mvinyo, wanywe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa BWANA, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenda kwa wazao wa Rekabu, useme nao. Kisha, uwalete katika chumba kimoja ndani ya nyumba yangu mimi Yawe, uwape divai wakunywe.