Jeremiah 35:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msijenge nyumba, msilime mashamba, wala msiwe na shamba la mizabibu. Lakini mtaishi katika mahema siku zote za maisha yenu, ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi mnamoishi kama wageni.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia msijenge nyumba wala kuotesha mbegu au kupanda mashamba ya mizabibu. Kamwe msiwe na kitu chochote katika hivi, bali mtaishi katika mahema. Ndipo mtakapoishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo ninyi ni wahamiaji.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema; mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake hali ya wageni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msijenge nyumba, msilime mashamba, wala msiwe na shamba la mizabibu. Lakini mtaishi katika mahema siku zote za maisha yenu, ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi mnamoishi kama wageni.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia msijenge nyumba kamwe, wala kuotesha mbegu au kupanda mashamba ya mizabibu, kamwe msiwe na kitu cho chote katika hivi, lakini siku zote lazima muishi kwenye mahema. Ndipo mtakapoishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo ninyi ni wahamiaji.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia msijenge nyumba kamwe, wala kuotesha mbegu au kupanda mashamba ya mizabibu. Kamwe msiwe na kitu chochote katika hivi, lakini siku zote lazima muishi kwenye mahema. Ndipo mtakapoishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo ninyi ni wahamiaji.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema; mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake kama wageni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msijenge nyumba, msilime mashamba, wala msiwe na shamba la mizabibu. Lakini mtaishi katika mahema siku zote za maisha yenu, ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi mnamoishi kama wageni.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala msijenge nyumba, wala msimwage mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo! Ila mkae mahemani siku zenu zote, mpate kuwapo siku nyingi huku nchini, mliko wageni ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema; mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake hali ya wageni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musijenge nyumba, musilime mashamba, wala musikuwe na shamba la mizabibu. Lakini mutaishi katika mahema siku zote za maisha yenu, kusudi mupate kuishi siku nyingi katika inchi munamoishi kama wageni.