Jeremiah 36:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, wakuu walimtuma Yehudi mwana wa Nethania, mjukuu wa Shelemia, kitukuu cha Kushi, amwambie Baruku hivi: “Chukua ile hati ya maandishi uliyosoma mbele ya watu uje nayo hapa.” Basi, Baruku mwana wa Neria, akachukua hati mkononi mwake, akawaendea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
maafisa wote wakamtuma Yehudi mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, kumwambia Baruku, “Leta hicho kitabu ambacho umewasomea watu, nawe mwenyewe uje.” Ndipo Baruku mwana wa Neria akawaendea akiwa na hicho kitabu mkononi mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wakuu wote wakamtuma Yehudi, mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, aende kwa Baruku, kumwambia, Litwae mkononi mwako gombo lile ulilolisoma masikioni mwa watu, uje huku. Basi, Baruku, mwana wa Neria, akalitwaa gombo lile mkononi mwake, akaenda kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, wakuu walimtuma Yehudi mwana wa Nethania, mjukuu wa Shelemia, kitukuu cha Kushi, amwambie Baruku hivi: “Chukua ile hati ya maandishi uliyosoma mbele ya watu uje nayo hapa.” Basi, Baruku mwana wa Neria, akachukua hati mkononi mwake, akawaendea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
maafisa wote wakamtuma Yehudi mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, kumwambia Baruki, “Leta hicho kitabu ambacho umewasomea watu nawe mwenyewe uje.” Ndipo Baruki mwana wa Neria akawaendea akiwa na hicho kitabu mkononi mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
maafisa wote wakamtuma Yehudi mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, kumwambia Baruku, “Leta hicho kitabu ambacho umewasomea watu, nawe mwenyewe uje.” Ndipo Baruku mwana wa Neria akawaendea akiwa na hicho kitabu mkononi mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wakuu wote wakamtuma Yehudi, mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, aende kwa Baruku, kumwambia, Litwae mkononi mwako gombo lile ulilolisoma masikioni mwa watu, uje huku. Basi, Baruku, mwana wa Neria, akalitwaa gombo lile mkononi mwake, akaenda kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, wakuu walimtuma Yehudi mwana wa Nethania, mjukuu wa Shelemia, kitukuu cha Kushi, amwambie Baruku hivi: “Chukua ile hati ya maandishi uliyosoma mbele ya watu uje nayo hapa.” Basi, Baruku mwana wa Neria, akachukua hati mkononi mwake, akawaendea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wakuu wote walipomtuma Yudi, mwana wa Netania, mwana wa Selemia, mwana wa Kusi, kwenda kwake Baruku kumwambia: Kitabu cha kuzingwa, ulichokisoma masikioni pao wa ukoo huu, kichukue mkononi mwako, uje huku! Baruku, mwana wa Neria, akakichukua kile kitabu cha kuzingwa mkononi mwake, akaja kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wakuu wote wakamtuma Yehudi, mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, aende kwa Baruku, kumwambia, Litwae mkononi mwako gombo lile ulilolisoma masikioni mwa watu, uje huku. Basi, Baruku, mwana wa Neria, akalitwaa gombo lile mkononi mwake, akaenda kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, wakubwa wakamutuma Yehudi mwana wa Netania, mujukuu wa Selemia, kijukuu cha Kusi, amwambie Baruku hivi: Twaa kile kitabu ulichosoma mbele ya watu ukuje nacho hapa. Basi, Baruku mwana wa Neria akatwaa kitabu katika mukono wake, akawaendea.