Jeremiah 36:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, mfalme alimtuma Yehudi aende kuleta ile hati. Yehudi aliichukua kutoka chumbani mwa katibu Elishama, akamsomea mfalme na wakuu wote waliokuwa wamesimama karibu na mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamtuma Yehudi akachukue kile kitabu. Yehudi akakileta hicho kitabu kutoka chumba cha Elishama mwandishi, na akakisoma mbele ya mfalme na maafisa wakiwa wamesimama kando ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, mfalme akamtuma Yehudi aende akalilete lile gombo; naye akalitoa katika chumba cha Elishama, mwandishi. Yehudi akalisoma masikioni mwa mfalme, na masikioni mwa wakuu waliosimama mbele ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, mfalme alimtuma Yehudi aende kuleta ile hati. Yehudi aliichukua kutoka chumbani mwa katibu Elishama, akamsomea mfalme na wakuu wote waliokuwa wamesimama karibu na mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akamtuma Yehudi akachukue kile kitabu na Yehudi akakileta hicho kitabu kutoka kwenye chumba cha Elishama mwandishi na akakisoma mbele ya mfalme na maafisa wakiwa wamesimama kando ya mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akamtuma Yehudi akachukue kile kitabu. Yehudi akakileta hicho kitabu kutoka kwenye chumba cha Elishama mwandishi, na akakisoma mbele ya mfalme na maafisa wakiwa wamesimama kando ya mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, mfalme akamtuma Yehudi aende akalilete lile gombo; naye akalitoa katika chumba cha Elishama, mwandishi. Yehudi akalisoma masikioni mwa mfalme, na masikioni mwa wakuu waliosimama mbele ya mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, mfalme alimtuma Yehudi aende kuleta ile hati. Yehudi aliichukua kutoka chumbani mwa katibu Elishama, akamsomea mfalme na wakuu wote waliokuwa wamesimama karibu na mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akamtuma Yudi kukichukua kile kitabu cha kuzingwa, akakichukua hicho kitabu katika ukumbi wa mwandishi Elisama, Yudi akakisoma masikioni pake mfalme napo masikioni pao wakuu wote waliosimama na kumzunguka mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, mfalme akamtuma Yehudi aende akalilete lile gombo; naye akalitoa katika chumba cha Elishama, mwandishi. Yehudi akalisoma masikioni mwa mfalme, na masikioni mwa wakuu waliosimama mbele ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mufalme alimutuma Yehudi aende kuleta kile kitabu. Yehudi alikitwaa kutoka ndani ya chumba cha katibu Elisama, akamusomea mufalme na wakubwa wote waliokuwa wamesimama karibu na mufalme.