Jeremiah 36:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ndani ya nyumba yake ya majira ya baridi, akiota moto wa makaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme alikuwa ameketi katika nyumba iliyotumika wakati wa baridi, mwezi wa kenda; na pale palikuwa na moto wa makaa mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ndani ya nyumba yake ya majira ya baridi, akiota moto wa makaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulikuwa mwezi wa tisa na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mfalme alikuwa ameketi katika nyumba iliyotumika wakati wa baridi, mwezi wa tisa; na pale palikuwa na moto wa makaa mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ndani ya nyumba yake ya majira ya baridi, akiota moto wa makaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mfalme akakaa katika nyumba ya kipupwe kwa kuwa mwezi wa tisa, nacho chano chenye makaa kikawaka moto mbele yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme alikuwa ameketi katika nyumba iliyotumika wakati wa baridi, mwezi wa kenda; na pale palikuwa na moto wa makaa mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo ulikuwa mwezi wa kenda, na mufalme alikuwa ndani ya nyumba yake ya nyakati za baridi. Mbele yake kulikuwa moto wa makaa.