Jeremiah 36:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu yake yeye Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Yeye hatakuwa na mzawa atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi, na maiti yake itatupwa nje kwenye joto mchana na baridi kali usiku.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Hatakuwa na mtu yeyote atakayekalia kiti cha utawala cha Daudi; maiti yake itatupwa nje kwenye joto wakati wa mchana na kupigwa na baridi wakati wa usiku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Bwana aseme hivi, katika habari za Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na mzoga wake utatupwa nje wakati wa mchana upigwe kwa hari, na wakati wa usiku upigwe kwa baridi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu yake yeye Yehoyakimu mfalme wa Yuda: yeye hatakuwa na mzawa atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi, na maiti yake itatupwa nje kwenye joto mchana na baridi kali usiku.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Hatakuwa na mtu ye yote atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi, maiti yake itatupwa nje kwenye joto wakati wa mchana na kupigwa na baridi wakati wa usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo bwana kuhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Hatakuwa na mtu yeyote atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi; maiti yake itatupwa nje kwenye joto wakati wa mchana na kupigwa na baridi wakati wa usiku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, BWANA aseme hivi, kuhusu Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na maiti yake itatupwa nje wakati wa mchana ipigwe na joto, na wakati wa usiku ipigwe na baridi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu yake yeye Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Yeye hatakuwa na mzawa atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi, na maiti yake itatupwa nje kwenye joto mchana na baridi kali usiku.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana anasema hivi kwa ajili ya Yoyakimu, mfalme wa Yuda: Hatampata atakayekaa katika kiti cha kifalme cha Dawidi, nao mzoga wake utakuwa umetupiwa jua kali la mchana nayo baridi ya usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, BWANA aseme hivi, katika habari za Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na mzoga wake utatupwa nje wakati wa mchana upigwe kwa hari, na wakati wa usiku upigwe kwa baridi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe anasema hivi juu yake yeye Yoyakimu mufalme wa Yuda: Yeye hatakuwa na mutu wa uzao wake atakayeikalia kiti cha kifalme cha Daudi, na maiti yake itatupwa inje kwenye joto muchana na baridi kali usiku.