Jeremiah 36:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria. Naye Baruku akaandika katika kitabu maneno yote aliyotamka Yeremia ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwambia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria, naye Yeremia alipokuwa akiyakariri maneno yote aliyoyasema Mwenyezi Mungu, Baruku akayaandika katika kitabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; naye Baruku akaandika katika gombo la chuo maneno yote ya Bwana, yaliyotoka kinywani mwa Yeremia, ambayo Bwana amemwambia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria. Naye Baruku akaandika katika kitabu maneno yote aliyotamka Yeremia ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwambia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yeremia akamwita Baruki mwana wa Neria, naye Yeremia alipokuwa akiyakariri maneno yote aliyoyasema BWANA, Baruki akayaandika katika kitabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria, naye Yeremia alipokuwa akiyakariri maneno yote aliyoyasema bwana, Baruku akayaandika katika kitabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; naye Baruku akaandika katika gombo la kitabu maneno yote ya BWANA, yaliyotoka kinywani mwa Yeremia, ambayo BWANA alikuwa amemwambia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria. Naye Baruku akaandika katika kitabu maneno yote aliyotamka Yeremia ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwambia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; kisha Baruku akayaandika katika kitabu cha kuzingwa maneno yote ya Bwana, aliyomwambia, kama Yeremia alivyoyasema kwa kinywa chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; naye Baruku akaandika katika gombo la chuo maneno yote ya BWANA, yaliyotoka kinywani mwa Yeremia, ambayo BWANA amemwambia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria. Naye Baruku akaandika katika kitabu maneno yote yaliyotoka katika kinywa cha Yeremia sawa vile Yawe alivyokuwa amemwambia.