Jeremiah 36:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mnamo siku ya kwanza ya mfungo, wewe utakwenda mbele ya umati wote wa watu, ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, usome hati ndefu ya maneno ya Mwenyezi-Mungu niliyokuamuru uandike kama nilivyoyasema. Utayasoma maneno hayo pia mbele ya watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wewe nenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu siku ya kufunga, uwasomee watu maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, enenda wewe, ukasome katika gombo la chuo, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya Bwana yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya Bwana, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda, watokao katika miji yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mnamo siku ya kwanza ya mfungo, wewe utakwenda mbele ya umati wote wa watu, ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, usome hati ndefu ya maneno ya Mwenyezi-Mungu niliyokuamuru uandike kama nilivyoyasema. Utayasoma maneno hayo pia mbele ya watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wewe nenda katika nyumba ya BWANA siku ya kufunga na uwasomee watu maneno ya BWANA kutoka katika kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka kwenye miji yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wewe nenda katika nyumba ya bwana siku ya kufunga, uwasomee watu maneno ya bwana kutoka kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, nenda wewe, ukasome katika gombo la kitabu, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya BWANA yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya BWANA, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda, watokao katika miji yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mnamo siku ya kwanza ya mfungo, wewe utakwenda mbele ya umati wote wa watu, ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, usome hati ndefu ya maneno ya Mwenyezi-Mungu niliyokuamuru uandike kama nilivyoyasema. Utayasoma maneno hayo pia mbele ya watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nenda, ukisome hiki kitabu, ulichokiandika maneno ya Bwana, kama nilivyoyasema kwa kinywa changu, watu wayasikie Nyumbani mwa Bwana siku ya kufunga mfungo, hata Wayuda wote waliokuja wakitoka mijini mwao sharti wayasikie, yakisomwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, enenda wewe, ukasome katika gombo la chuo, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya BWANA yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya BWANA, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda, watokao katika miji yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa siku ya kwanza ya kufunga kula chakula, wewe utakwenda mbele ya watu wote, ndani ya nyumba ya Yawe, usome kitabu chenye maneno ya Yawe uliyoyaandika kutoka katika kinywa changu. Utayasoma maneno hayo mbele ya watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao vilevile.