Jeremiah 36:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Labda maombi yao yatamfikia Mwenyezi-Mungu na kwamba kila mmoja wao ataacha mwenendo wake mwovu kwa maana Mwenyezi-Mungu ametamka adhabu dhidi ya watu hawa kwa hasira na ghadhabu kali.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Labda wataomba na kusihi mbele za Mwenyezi Mungu na kila mmoja akageuka kutoka njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na Mwenyezi Mungu ni kubwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Labda wataomba dua zao mbele za Bwana, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; kwa maana hasira na ghadhabu ni kuu sana, alizotamka Bwana juu ya watu hawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Labda maombi yao yatamfikia Mwenyezi-Mungu na kwamba kila mmoja wao ataacha mwenendo wake mwovu kwa maana Mwenyezi-Mungu ametamka adhabu dhidi ya watu hawa kwa hasira na ghadhabu kali.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Labda wataomba na kusihi mbele za BWANA na kila mmoja atageuka kutoka katika njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na BWANA ni kubwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Labda wataomba na kusihi mbele za bwana na kila mmoja akageuka kutoka njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na bwana ni kubwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Labda wataomba dua zao mbele za BWANA, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; kwa maana hasira na ghadhabu ni kuu sana, alizotamka BWANA juu ya watu hawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Labda maombi yao yatamfikia Mwenyezi-Mungu na kwamba kila mmoja wao ataacha mwenendo wake mwovu kwa maana Mwenyezi-Mungu ametamka adhabu dhidi ya watu hawa kwa hasira na ghadhabu kali.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Labda malalamiko yao yatamwangukia Bwana usoni pake, wakirudi kila mtu katika njia zake mbaya, kwani makali yenye moto ni makuu, Bwana aliyoyasema kuwafanyizia watu wa ukoo huu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Labda wataomba dua zao mbele za BWANA, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; kwa maana hasira na ghadhabu ni kuu sana, alizotamka BWANA juu ya watu hawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labda maombi yao yatamufikia Yawe na kila mumoja wao ataacha mwenendo wake mubaya kwa maana hasira na kasirani ambavyo Yawe amesema juu ya watu hawa ni kubwa sana.