Jeremiah 38:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati fulani mfalme Sedekia alitaka kumwona nabii Yeremia. Basi, akaagiza Yeremia aletwe kwenye mlango wa tatu wa hekalu la Mwenyezi-Mungu. Huko, mfalme alimwambia Yeremia, “Nataka kukuuliza jambo fulani; usinifiche kitu chochote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mfalme Sedekia akatuma watu wamwitie nabii Yeremia wamlete kwake kwenye ingilio la tatu la Hekalu la Mwenyezi Mungu. Mfalme akamwambia Yeremia, “Ninataka kukuuliza jambo fulani, usinifiche kitu chochote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mfalme Sedekia akatuma watu, akamleta nabii Yeremia kwake, ndani ya maingilio ya tatu ya nyumba ya Bwana; mfalme akamwambia Yeremia, Nataka kukuuliza neno, nawe usinifiche neno lo lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati fulani mfalme Sedekia alitaka kumwona nabii Yeremia. Basi, akaagiza Yeremia aletwe kwenye mlango wa tatu wa hekalu la Mwenyezi-Mungu. Huko, mfalme alimwambia Yeremia, “Nataka kukuuliza jambo fulani; usinifiche kitu chochote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mfalme Sedekia akatuma wamwitie nabii Yeremia na kutaka wamlete kwake kwenye ingilio la tatu kwenye Hekalu la BWANA. Mfalme akamwambia Yeremia, “Ninataka kukuuliza jambo fulani, usinifiche kitu cho chote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Mfalme Sedekia akatuma watu wamwitie nabii Yeremia wamlete kwake kwenye ingilio la tatu la Hekalu la bwana. Mfalme akamwambia Yeremia, “Ninataka kukuuliza jambo fulani, usinifiche kitu chochote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mfalme Sedekia akatuma watu, akamleta nabii Yeremia kwake, ndani ya maingilio ya tatu ya nyumba ya BWANA; mfalme akamwambia Yeremia, Nataka kukuuliza neno, nawe usinifiche neno lolote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati fulani mfalme Sedekia alitaka kumwona nabii Yeremia. Basi, akaagiza Yeremia aletwe kwenye mlango wa tatu wa hekalu la Mwenyezi-Mungu. Huko, mfalme alimwambia Yeremia, “Nataka kukuuliza jambo fulani; usinifiche kitu chochote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme Sedekia akatuma kumchukua mfumbuaji Yeremia, aje kwake penye lango la tatu la kuiingilia Nyumba ya Bwana, mfalme akamwambia Yeremia: Mimi ninataka kukuuliza neno, lakini usinifiche lo lote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mfalme Sedekia akatuma watu, akamleta nabii Yeremia kwake, ndani ya maingilio ya tatu ya nyumba ya BWANA; mfalme akamwambia Yeremia, Nataka kukuuliza neno, nawe usinifiche neno lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati fulani mufalme Zedekia alitaka kumwona nabii Yeremia. Basi, akaagiza Yeremia aletwe kwenye mulango wa tatu wa nyumba ya Yawe. Huko, mufalme alimwambia Yeremia: Ninataka kukuuliza jambo fulani; usinifiche kitu chochote.