Jeremiah 38:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yeremia akamwambia Sedekia: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kama ukijitoa mwenyewe na kujitia mikononi mwa maofisa wa mfalme wa Babuloni, utayaokoa maisha yako na mji hautateketezwa kwa moto; nawe pamoja na jamaa yako mtaendelea kuishi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika, na mji huu hautateketezwa kwa moto. Pia wewe na jamaa yako mtaishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yeremia akamwambia Sedekia: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kama ukijitoa mwenyewe na kujitia mikononi mwa maofisa wa mfalme wa Babuloni, utayaokoa maisha yako na mji hautateketezwa kwa moto; nawe pamoja na jamaa yako mtaendelea kuishi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika na mji huu hautateketezwa kwa moto, wewe na jamaa yako mtaishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika, na mji huu hautateketezwa kwa moto. Pia wewe na jamaa yako mtaishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yeremia akamwambia Sedekia: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kama ukijitoa mwenyewe na kujitia mikononi mwa maofisa wa mfalme wa Babuloni, utayaokoa maisha yako na mji hautateketezwa kwa moto; nawe pamoja na jamaa yako mtaendelea kuishi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yeremia alipomwambia Sedekia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Kama utawatokea wakuu wa mfalme wa Babeli, roho yako itapona, nao mji huu hautateketezwa kwa moto; hivyo utapona wewe na mlango wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo Yeremia akamwambia Zedekia: Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kama ukijitoa mwenyewe na kujitia katika mikono ya wakubwa wa mufalme wa Babeli, utayaokoa maisha yako na muji hautateketezwa kwa moto; nawe pamoja na jamaa yako mutaendelea kuishi.