Jeremiah 38:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, viongozi walimjia Yeremia wakamwuliza mambo hayo, naye akawajibu kama mfalme alivyomwelekeza. Ndipo walipoacha kuzungumza naye kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa amesikia mazungumzo yake na mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Viongozi wote wakamjia Yeremia na kumuuliza, naye Yeremia akawaambia kila kitu mfalme alichomwagiza kusema. Kisha hawakusema lolote zaidi na Yeremia kwa sababu hakuna hata mmoja aliyekuwa amesikia mazungumzo yake na mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, viongozi walimjia Yeremia wakamwuliza mambo hayo, naye akawajibu kama mfalme alivyomwelekeza. Ndipo walipoacha kuzungumza naye kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa amesikia mazungumzo yake na mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wote wakamjia Yeremia na kumwuliza, naye Yeremia akawaambia kila kitu mfalme alichomwagiza kusema. Kisha hawakusema lo lote zaidi na Yeremia kwa sababu hakuna ye yote aliyesikia mazungumzo yake na mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wote wakamjia Yeremia na kumuuliza, naye Yeremia akawaambia kila kitu mfalme alichomwagiza kusema. Kisha hawakusema lolote zaidi na Yeremia kwa sababu hakuna yeyote aliyesikia mazungumzo yake na mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, viongozi walimjia Yeremia wakamwuliza mambo hayo, naye akawajibu kama mfalme alivyomwelekeza. Ndipo walipoacha kuzungumza naye kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa amesikia mazungumzo yake na mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wakaja kwake Yeremia, wakamwuliza, akawaambia hayo maneno yote, kama mfalme alivyomwagiza, wakamwacha na kunyamaza, kwani lile shauri halikujulikana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, wakubwa walimufikia Yeremia wakamwuliza mambo hayo, naye akawajibu kama vile mufalme alivyomwelekeza. Halafu waliacha kuzungumuza naye kwa sababu hakuna mutu aliyekuwa amesikia mazungumuzo yake na mufalme.