Jeremiah 38:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamchukua Yeremia wakamtumbukiza katika kisima cha Malkia mwana wa mfalme ambacho kilikuwa katika ukumbi wa walinzi. Walimshusha Yeremia ndani kwa kamba. Ndani ya kisima hicho hakukuwa na maji bali tope, naye Yeremia akazama katika tope.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wakamchukua Yeremia na kumtia kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme, kilichokuwa katika ua wa walinzi. Wakamteremsha Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. Hakikuwa na maji ndani yake, ila tope tu, naye Yeremia akazama ndani ya matope.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamchukua Yeremia wakamtumbukiza katika kisima cha Malkia mwana wa mfalme ambacho kilikuwa katika ukumbi wa walinzi. Walimshusha Yeremia ndani kwa kamba. Ndani ya kisima hicho hakukuwa na maji bali tope, naye Yeremia akazama katika tope.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wakamchukua Yeremia na kumtia kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme, kilichokuwa katika ua wa walinzi. Wakamtelemsha Yeremia kwa kamba ndani ya kisima, hakikuwa na maji ndani yake, ila tope tu, naye Yeremia akazama ndani ya matope.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wakamchukua Yeremia na kumtia kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme, kilichokuwa katika ua wa walinzi. Wakamteremsha Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. Hakikuwa na maji ndani yake, ila tope tu, naye Yeremia akazama ndani ya matope.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika ukumbi wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamchukua Yeremia wakamtumbukiza katika kisima cha Malkia mwana wa mfalme ambacho kilikuwa katika ukumbi wa walinzi. Walimshusha Yeremia ndani kwa kamba. Ndani ya kisima hicho hakukuwa na maji bali tope, naye Yeremia akazama katika tope.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamchukua Yeremia, wakamtupa katika kisima cha Malkia, mwana wa mfalme, kilichokuwa hapo uani penye kifungo, wakamshusha Yeremia mle kwa kamba. Mle kisimani hamkuwa na maji, ila ni matopetope tu, Yeremia akaanza kuzama matopeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakamutwaa Yeremia wakamutia katika kisima cha Malkia mwana wa mufalme ambacho kilikuwa katika kiwanja cha walinzi. Walimushusha Yeremia ndani kwa kamba. Ndani ya kisima hicho hamukukuwa maji lakini matope, naye Yeremia akazama katika matope.