Jeremiah 38:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Bwana wangu mfalme, watu hawa wamefanya kitu kibaya. Wamemtumbukiza yule nabii Yeremia kisimani ambamo kwa kweli atakufa kwa njaa, kwa maana hamna chakula tena mjini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mfalme bwana wangu, watu hawa wamefanya uovu kwa yote waliomtendea nabii Yeremia. Wamemtupa ndani ya kisima, ambamo atakufa kwa njaa chakula kitakapokosekana katika mji.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hapana mkate kabisa katika mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Bwana wangu mfalme, watu hawa wamefanya kitu kibaya. Wamemtumbukiza yule nabii Yeremia kisimani ambamo kwa kweli atakufa kwa njaa, kwa maana hamna chakula tena mjini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mfalme bwana wangu, watu hawa wamefanya uovu kwa yote waliomtendea nabii Yeremia. Wamemtupa ndani ya kisima, mahali ambapo atakufa kwa njaa wakati ambapo hakuna chakula po pote katika mji.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mfalme bwana wangu, watu hawa wamefanya uovu kwa yote waliomtendea nabii Yeremia. Wamemtupa ndani ya kisima, mahali ambapo atakufa kwa njaa wakati ambapo hakuna chakula popote katika mji.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hakuna mkate kabisa katika mji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Bwana wangu mfalme, watu hawa wamefanya kitu kibaya. Wamemtumbukiza yule nabii Yeremia kisimani ambamo kwa kweli atakufa kwa njaa, kwa maana hamna chakula tena mjini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana wangu mfalme, yote, watu waliyomfanyizia mfumbuaji Yeremia, ni mabaya, wakimtupa kisimani, afie mle ndani kwa njaa, kwani hamna mkate tena humu mjini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hapana mkate kabisa katika mji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wangu mufalme, watu hawa wamefanya kitu kibaya. Wamemutia yule nabii Yeremia katika kisima ambamo kwa kweli atakufa kwa njaa, kwa maana hakuna chakula tena katika muji.