Jeremiah 39:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwezi wa tisa wa mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babuloni alifika na jeshi lake lote kuushambulia mji wa Yerusalemu, akauzingira.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu na akauzingira.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa kenda wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauhusuru;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwezi wa tisa wa mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babuloni alifika na jeshi lake lote kuushambulia mji wa Yerusalemu, akauzingira.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa: Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alilipeleka jeshi lake lote dhidi ya Yerusalemu na akauzunguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa: Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu na akauzunguka mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa tisa wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauzingira;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo mwezi wa tisa wa mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babuloni alifika na jeshi lake lote kuushambulia mji wa Yerusalemu, akauzingira.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yerusalemu ukatekwa hivyo: katika mwaka wa 9 wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa 9 Nebukadinesari, mfalme wa Babeli alikuja Yerusalemu na vikosi vyake vyote, wakaanza kuusonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa kenda wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauhusuru;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwezi wa kenda wa mwaka wa kenda wa utawala wa Zedekia mufalme wa Yuda, Nebukadneza mufalme wa Babeli alifika na waaskari wake wote kuushambulia Yerusalema, akauzunguka kwa vita.