Jeremiah 39:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwaacha katika nchi ya Yuda baadhi ya watu maskini ambao hawakuwa na chochote, akawagawia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na makonde wakati uo huo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwaacha katika nchi ya Yuda baadhi ya watu maskini ambao hawakuwa na chochote, akawagawia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Nebuzaradani, kiongozi wa walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu, naye kwa wakati ule aliwapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Nebuzaradani kiongozi wa walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba wakati huo huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwaacha katika nchi ya Yuda baadhi ya watu maskini ambao hawakuwa na chochote, akawagawia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini waliokuwa wanyonge wa ukoo huu, wasiokuwa na kitu, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akawaacha katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine siku ile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na makonde wakati uo huo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nebuzaradani, mukubwa wa walinzi wa mufalme, aliwaacha katika inchi ya Yuda watu wamoja wamasikini ambao hawakukuwa na kitu chochote, akawagawanyia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.