Jeremiah 39:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nenda ukamwambie hivi Ebedmeleki, Mwethiopia: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama mimi nitatimiza mambo yale niliyotamka dhidi ya mji huo na sio mambo mema. Mambo hayo yatakamilika siku hiyo ukiona wewe mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nenda ukamwambie Ebed-Meleki Mkushi, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kutimiza maneno yangu dhidi ya mji huu kwa maafa, wala si kwa mema. Wakati huo, hayo yatatimizwa mbele ya macho yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya! Enenda ukaseme na Ebedmeleki, Mkushi, kusema, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaupatiliza mji huu maneno yangu kwa mabaya, wala si kwa mema; nayo yatatimizwa mbele yako katika siku hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nenda ukamwambie hivi Ebedmeleki, Mwethiopia: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama mimi nitatimiza mambo yale niliyotamka dhidi ya mji huo na sio mambo mema. Mambo hayo yatakamilika siku hiyo ukiona wewe mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nenda ukamwambie Ebed-Meleki, Mkushi, ‘Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kutimiza maneno yangu dhidi ya mji huu kwa njia ya maafa, wala si kwa kuwafanikisha. Wakati huo hayo yatatimizwa mbele ya macho yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nenda ukamwambie Ebed-Meleki Mkushi, ‘Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kutimiza maneno yangu dhidi ya mji huu kwa njia ya maafa, wala si kwa kuwafanikisha. Wakati huo hayo yatatimizwa mbele ya macho yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya! Nenda ukaseme na Ebedmeleki, Mkushi, kusema, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaupatiliza mji huu kwa maneno yangu mabaya, wala si kwa mema; nayo yatatimizwa mbele yako katika siku hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nenda ukamwambie hivi Ebedmeleki, Mwethiopia: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama mimi nitatimiza mambo yale niliyotamka dhidi ya mji huo na sio mambo mema. Mambo hayo yatakamilika siku hiyo ukiona wewe mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nenda kumwambia Ebedimeleki, yule Mnubi, kwamba: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Utaniona, nikiuletea mji huu niliyoyasema, yauwie, nayo ni mabaya, siyo mema, yatatimia usoni pako siku ile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya! Enenda ukaseme na Ebedmeleki, Mkushi, kusema, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaupatiliza mji huu maneno yangu kwa mabaya, wala si kwa mema; nayo yatatimizwa mbele yako katika siku hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenda kwa Ebedimeleki Mwetiopia umwambie hivi: Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Angalia mimi nitatimiza mambo yale niliyosema juu ya muji huo na sio mambo mema. Mambo hayo yatakamilika siku hiyo ukiona wewe mwenyewe.