Jeremiah 39:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini jeshi la Wakaldayo liliwafuatia na kumteka Sedekia katika tambarare za Yeriko. Baada ya kumchukua walimfikisha kwa Nebukadneza, mfalme wa Babuloni huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, naye akamhukumu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia na kumpata Sedekia katika nchi tambarare za Yeriko. Wakamkamata na kumpeleka kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ambapo alimtangazia hukumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko; nao walipomkamata, wakamleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini jeshi la Wakaldayo liliwafuatia na kumteka Sedekia katika tambarare za Yeriko. Baada ya kumchukua walimfikisha kwa Nebukadneza, mfalme wa Babuloni huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, naye akamhukumu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini jeshi la Wakaldayo liliwafuatia na kumkuta Sedekia kwenye tambarare za Yeriko. Wakamkamata na kumpeleka kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli huko Ribla katika nchi ya Hamathi, mahali walipomhukumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini jeshi la Wakaldayo likawafuatia na kumpata Sedekia katika sehemu tambarare za Yeriko. Wakamkamata na kumpeleka kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mahali ambapo alimtangazia hukumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko; nao walipomkamata, wakamleta kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini jeshi la Wakaldayo liliwafuatia na kumteka Sedekia katika tambarare za Yeriko. Baada ya kumchukua walimfikisha kwa Nebukadneza, mfalme wa Babuloni huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, naye akamhukumu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vikosi vya Wakasidi vikawafuata na kupiga mbio, wakamfikia Sedekia katika nyika ya Yeriko, wakamkamata, wakampeleka kwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, mjini mwa Ribula katika nchi ya Hamati, yeye akasema naye na kumhukumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko; nao walipomkamata, wakamleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kundi la waaskari la Wakaldea liliwafuatilia na kumukamata Zedekia karibu na Yeriko. Kisha kumukamata walimufikisha kwa Nebukadneza, mufalme wa Babeli huko Ribla, katika inchi ya Hamati, naye akamuhukumu.