Jeremiah 4:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, wataambiwa hivi watu hawa pamoja na mji wa Yerusalemu, “Upepo wa hari kutoka vilele vikavu vya jangwani utawavumia watu wangu. Huo si upepo wa kupepeta au kusafisha,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame jangwani unavuma kuelekea kwa watu wangu, lakini sio upepo wa kupepeta na kutakasa;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati ule watu hawa na Yerusalemu wataambiwa neno hili, Upepo wa moto utokao katika vilele vya nyikani visivyo na miti, ukimwelekea binti ya watu wangu, hauwi upepo wa kupepeta, wala upepo wa kutakasa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, wataambiwa hivi watu hawa pamoja na mji wa Yerusalemu, “Upepo wa hari kutoka vilele vikavu vya jangwani utawavumia watu wangu. Huo si upepo wa kupepeta au kusafisha,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati ule watu hawa na Yerusalemu wataambiwa neno hili, Upepo wa moto utokao katika vilele vya nyikani visivyo na miti, ukimwelekea binti ya watu wangu, hauwi upepo wa kupepeta, wala upepo wa kutakasa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, wataambiwa hivi watu hawa pamoja na mji wa Yerusalemu, “Upepo wa hari kutoka vilele vikavu vya jangwani utawavumia watu wangu. Huo si upepo wa kupepeta au kusafisha,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile watu wa ukoo huu nao Wayerusalemu wataambiwa: Upepo uchomao moto umetoka vilimani nyikani, ukaja kuwavumia wazaliwa wa ukoo wangu, sio wa kupunga wala wa kupepeta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati ule watu hawa na Yerusalemu wataambiwa neno hili, Upepo wa moto utokao katika vilele vya nyikani visivyo na miti, ukimwelekea binti ya watu wangu, hauwi upepo wa kupepeta, wala upepo wa kutakasa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo, wataambiwa hivi watu hawa pamoja na muji Yerusalema: Upepo wenye kuunguza kutoka vilele vya milima katika jangwa utawavumia watu wangu. Huo si upepo mudogo wa kupepeta ngano,