Jeremiah 4:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliona nchi yenye rutuba imekuwa jangwa, na miji yake yote imekuwa magofu matupu, kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilitazama, nayo nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa, miji yake yote ilikuwa magofu mbele za Mwenyezi Mungu, mbele ya hasira yake kali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliona nchi yenye rutuba imekuwa jangwa, na miji yake yote imekuwa magofu matupu, kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa, miji yake yote ilikuwa magofu mbele za BWANA, mbele ya hasira yake kali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa, miji yake yote ilikuwa magofu mbele za bwana, mbele ya hasira yake kali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za BWANA, na mbele za hasira yake kali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliona nchi yenye rutuba imekuwa jangwa, na miji yake yote imekuwa magofu matupu, kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikatazama, nikaona, ya kuwa mashamba yenye matunda ni nyika, nayo miji yao yote ilikuwa imebomolewa, Bwana asiione tena kwa kuwa na makali yenye moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za BWANA, na mbele za hasira yake kali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliona inchi yote yenye mboleo imegeuka jangwa, nayo miji yake yote imebaki mabomoko matupu, kwa sababu ya hasira kali ya Yawe.