Jeremiah 4:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watakaposikika wapandafarasi na wapiga mishale, kila mmoja atatimua mbio. Baadhi yao watakimbilia msituni, wengine watapanda majabali. Kila mji utaachwa tupu; hakuna mtu atakayekaa ndani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde kila mji unakimbia. Baadhi wanakimbilia vichakani, baadhi wanapanda juu ya miamba. Miji yote imeachwa, hakuna aishiye ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mji mzima unakimbia, kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi na wenye pinde wanaingia vichakani, wanapanda juu ya majabali; kila mji umeachwa, hapana hata mtu mmoja akaaye ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watakaposikika wapandafarasi na wapiga mishale, kila mmoja atatimua mbio. Baadhi yao watakimbilia msituni, wengine watapanda majabali. Kila mji utaachwa tupu; hakuna mtu atakayekaa ndani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde kila mji unakimbia. Baadhi wanakimbilia vichakani, baadhi wanapanda juu ya miamba. Miji yote imeachwa, hakuna aishiye ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde kila mji unakimbia. Baadhi wanakimbilia vichakani, baadhi wanapanda juu ya miamba. Miji yote imeachwa, hakuna aishiye ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mji mzima unakimbia, kwa sababu ya kishindo cha wapanda farasi na wenye pinde wanaingia vichakani, wanapanda juu ya majabali; kila mji umeachwa, hakuna hata mtu mmoja akaaye ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watakaposikika wapandafarasi na wapiga mishale, kila mmoja atatimua mbio. Baadhi yao watakimbilia msituni, wengine watapanda majabali. Kila mji utaachwa tupu; hakuna mtu atakayekaa ndani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa makelele yao wapanda farasi na wenye kuvuta pindi watu wote waliomo mijini wamekimbia, wakaingia machakani, wakapanda magengeni, miji yote ikaachwa, hakuna mtu anayekaa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mji mzima unakimbia, kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi na wenye pinde wanaingia vichakani, wanapanda juu ya majabali; kila mji umeachwa, hapana hata mtu mmoja akaaye ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kelele la waaskari wapanda-farasi na la wapiga mishale litakaposikilika, watu wote watakimbia. Wamoja wao watakimbilia katika vichaka, wengine watajificha katikati ya mawe. Kila muji utaachwa tupu; hakuna mutu atakayekaa ndani yake.