Jeremiah 4:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawe Yerusalemu uliyeachwa tupu, unavalia nini mavazi mekundu? Ya nini kujipamba kwa dhahabu, na kujipaka wanja machoni? Unajirembesha bure! Wapenzi wako wanakudharau sana; wanachotafuta ni kukuua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa? Kwa nini unajivika vazi jekundu na kuvaa vito vya dhahabu? Kwa nini unapaka macho yako wanja? Unajipamba bure. Wapenzi wako wanakudharau, wanautafuta uhai wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawe Yerusalemu uliyeachwa tupu, unavalia nini mavazi mekundu? Ya nini kujipamba kwa dhahabu, na kujipaka wanja machoni? Unajirembesha bure! Wapenzi wako wanakudharau sana; wanachotafuta ni kukuua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa? Kwa nini unajivika vazi jekundu na kuvaa vito vya dhahabu? Kwa nini unapaka macho yako rangi? Unajipamba bure. Wapenzi wako wanakudharau, wanautafuta uhai wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa? Kwa nini unajivika vazi jekundu na kuvaa vito vya dhahabu? Kwa nini unapaka macho yako rangi? Unajipamba bure. Wapenzi wako wanakudharau, wanautafuta uhai wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawe Yerusalemu uliyeachwa tupu, unavalia nini mavazi mekundu? Ya nini kujipamba kwa dhahabu, na kujipaka wanja machoni? Unajirembesha bure! Wapenzi wako wanakudharau sana; wanachotafuta ni kukuua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe ukiharibiwa hivyo utafanyaje? Ijapo uvae nguo nyekundu za kifalme, ujipambe mapambo ya dhahabu, hata utie wanja machoni pako, huo uzuri wako utakuwa wa bure, wapenzi wako watakubeza, tamaa zao ni kukuua tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe Yerusalema uliyeachwa tupu, kwa nini sasa unavaa nguo nzuri nyekundu? Kwa nini kujipamba kwa zahabu, na kujipakaa wanja kwenye macho? Unajipamba bure! Wapenzi wako wanakuzarau sana; wanatafuta kukuua tu.