Jeremiah 4:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilisikia sauti kama ya mwanamke anayejifungua, yowe kama anayejifungua mtoto wa kwanza. Ilikuwa sauti ya Yerusalemu akitweta, na kuinyosha mikono yake akisema, ‘Ole wangu! Wanakuja kuniua!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nasikia kilio kama cha mwanamke katika uchungu wa kuzaa, kilio cha uchungu kama cha anayemzaa mtoto wake wa kwanza: kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua, akiinua mikono yake, akisema, “Ole wangu! Ninazimia; maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa utungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilisikia sauti kama ya mwanamke anayejifungua, yowe kama anayejifungua mtoto wa kwanza. Ilikuwa sauti ya Yerusalemu akitweta, na kuinyosha mikono yake akisema, ‘Ole wangu! Wanakuja kuniua!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nasikia kilio kama cha mwanamke aliye katika utungu wa kuzaa, kilio cha uchungu kama cha anayemzaa mtoto wake wa kwanza: kilio cha Binti Sayuni akitapatapa ili aweze kupumua, akiinua mikono yake, akisema, “Ole wangu! Ninazimia; maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nasikia kilio kama cha mwanamke katika utungu wa kuzaa, kilio cha uchungu kama cha anayemzaa mtoto wake wa kwanza: kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua, akiinua mikono yake, akisema, “Ole wangu! Ninazimia; maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilisikia sauti kama ya mwanamke anayejifungua, yowe kama anayejifungua mtoto wa kwanza. Ilikuwa sauti ya Yerusalemu akitweta, na kuinyosha mikono yake akisema, ‘Ole wangu! Wanakuja kuniua!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimesikia sauti kama ya mwanamke mwenye kuzaa aonaye uchungu zaidi kwa kuzaa mara ya kwanza, ni sauti ya binti Sioni, akipiga kite na kuikunjua mikono yake kwamba: A, yamenipata! Roho yangu inazimia mbele yao wauao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa utungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilisikia sauti kama ya mwanamuke anayezaa, malalamiko kama ya mwenye kuzaa mutoto wa kwanza. Ilikuwa sauti ya Yerusalema akipumuapumua kwa uchungu, na kuinyooshanyoosha mikono yake, akisema: Ole wangu! Wanakuja kuniua!