Jeremiah 4:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Twekeni bendera ya vita kuelekea Siyoni, kimbilieni usalama wenu, msisitesite! Mwenyezi-Mungu analeta maafa na maangamizi makubwa kutoka kaskazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inueni ishara ili kwenda Sayuni! Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa! Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini, maangamizi ya kutisha.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamivu makuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Twekeni bendera ya vita kuelekea Siyoni, kimbilieni usalama wenu, msisitesite! Mwenyezi-Mungu analeta maafa na maangamizi makubwa kutoka kaskazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni! Kimbilieni kwenye usalama pasipo kuchelewa! Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini, yaani maangamizi ya kutisha.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni! Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa! Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini, maangamizi ya kutisha.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamizi makuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Twekeni bendera ya vita kuelekea Siyoni, kimbilieni usalama wenu, msisitesite! Mwenyezi-Mungu analeta maafa na maangamizi makubwa kutoka kaskazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Twekeni bendera, ielekee Sioni! Jihimizeni kukimbia, msisimame! Kwani mimi ninaleta mabaya kutoka upande wa kaskazini, hata mavunjiko mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamivu makuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muinue bendera ya vita kuelekea Sayuni, kusudi mukimbie, wala musisitesite! Yawe analeta hasara, analeta maangamizi makubwa kutoka kaskazini.