Jeremiah 4:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika siku hiyo itakuwa, asema Bwana, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Katika siku ile,” asema BWANA “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Katika siku ile,” asema bwana “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Itakuwa, siku ile moyo wa mfalme utapotea pamoja na mioyo ya wakuu wake, nao watambikaji watastuka, hata wafumbuaji watapigwa na bumbuazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, mufalme na wakubwa wataregea moyo. Makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa. –Ni ujumbe wa Yawe.