Jeremiah 40:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu wakati Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alipomruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo kapteni alimchukua Yeremia amefungwa minyororo, akawachukua pia pamoja naye mateka wengine wote wa Yerusalemu na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa uhamishoni Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno likamjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, baada ya wakati ule Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua hali ya kufungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa hali ya kufungwa mpaka Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu wakati Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alipomruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo kapteni alimchukua Yeremia amefungwa minyororo, akawachukua pia pamoja naye mateka wengine wote wa Yerusalemu na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa uhamishoni Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neno likamjia Yeremia kutoka kwa BWANA baada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa kifalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neno likamjia Yeremia kutoka kwa bwana baada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu wakati Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, alipomruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo kapteni alimchukua Yeremia amefungwa minyororo, akawachukua pia pamoja naye mateka wengine wote wa Yerusalemu na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa uhamishoni Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, alipompa ruhusa huko Rama kujiendea; naye alimpata, alipokuwa amefungwa kwa minyororo, katikati ya mateka yote ya Yerusalemu na ya Yuda waliokwenda kupelekwa Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua hali ya kufungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa hali ya kufungwa mpaka Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huu ni ujumbe uliotolewa kwa Yeremia kutoka kwa Yawe wakati Nebuzaradani mukubwa wa walinzi wa mufalme alipomuruhusu Yeremia aondoke Rama. Huyo mukubwa alimukamata Yeremia akifungwa minyororo, pamoja na wafungwa wengine wote wa Yerusalema na Yuda ambao walikuwa wamepelekwa katika uhamisho kule Babeli.