Jeremiah 40:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Yohanani mwana wa Karea, akazungumza na Gedalia kwa faragha huko Mizpa, akamwambia, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, na hakuna mtu yeyote atakayejua. Kwa nini yeye akuue na watu wa Yuda wote waliokusanyika hapa watawanyike na Wayahudi waliobaki waangamie?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko Mispa, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokuzunguka watawanyike, na mabaki wa Yuda waangamie?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Yohana, mwana wa Karea, akamwambia Gedalia huko Mizpa kwa siri, akisema, Niache niende nikampige Ishmaeli, mwana wa Nethania, wala hapana mtu atakayejua jambo hili; kwani akuue wewe, hata wakatawanyike Wayahudi waliokukusanyikia, na mabaki ya Yuda wakaangamie?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Yohanani mwana wa Karea, akazungumza na Gedalia kwa faragha huko Mizpa, akamwambia, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, na hakuna mtu yeyote atakayejua. Kwa nini yeye akuue na watu wa Yuda wote waliokusanyika hapa watawanyike na Wayahudi waliobaki waangamie?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko katika Mizpa. “Acha niende nikamwue Ishmaeli mwana wa Nethania wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokusanyika kukuzunguka watawanyike na mabaki wa Yuda waangamie?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko Mispa, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokuzunguka watawanyike, na mabaki wa Yuda waangamie?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, Yohana, mwana wa Karea, akamwambia Gedalia huko Mizpa kwa siri, akisema, Niache niende nikampige Ishmaeli, mwana wa Nethania, wala hapana mtu atakayejua jambo hili; kwa nini akuue wewe, hata wakatawanyike Wayahudi waliokukusanyikia, na mabaki ya Yuda wakaangamie?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Yohanani mwana wa Karea, akazungumza na Gedalia kwa faragha huko Mizpa, akamwambia, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, na hakuna mtu yeyote atakayejua. Kwa nini yeye akuue na watu wa Yuda wote waliokusanyika hapa watawanyike na Wayahudi waliobaki waangamie?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yohana, mwana wa Karea, alipomwambia Gedalia penye njama huko Misipa kwamba: Na niende, nimwue Isimaeli, mwana wa Netania, mtu asijue! Kwa nini akuue wewe mwenyewe, Wayuda wote waliokusanyika kwako watawanyike tena, hayo masao ya Yuda yaangamie?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, Yohana, mwana wa Karea, akamwambia Gedalia huko Mizpa kwa siri, akisema, Niache niende nikampige Ishmaeli, mwana wa Nethania, wala hapana mtu atakayejua jambo hili; kwani akuue wewe, hata wakatawanyike Wayahudi waliokukusanyikia, na mabaki ya Yuda wakaangamie?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Yohana mwana wa Karea akazungumuza na Gedalia kwa siri kule Misipa, akamwambia: Uniruhusu niende nimwue Isimaeli mwana wa Netania, na hakuna mutu yeyote atakayejua. Kwa nini kumwachilia yeye akuue na Wayuda wote waliokusanyika hapa watawanyike na Wayuda waliobaki waangamie?