Jeremiah 40:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya! Leo nazifungua pingu mikononi mwako. Kama unaona ni vema kwenda pamoja nami mpaka Babuloni, basi twende pamoja; mimi nitakutunza vizuri. Lakini kama unaona si vizuri kwako kwenda pamoja nami mpaka Babuloni, basi, usije. Ujue kwamba waweza kwenda popote katika nchi hii; basi nenda popote unapoamua kuwa pazuri kwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini leo ninakufungua minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Ukiona ni vema, twende pamoja hadi Babeli; nami nitakutunza. Lakini kama hutaki, basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda kokote unakotaka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote i mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, enenda huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya! Leo nazifungua pingu mikononi mwako. Kama unaona ni vema kwenda pamoja nami mpaka Babuloni, basi twende pamoja; mimi nitakutunza vizuri. Lakini kama unaona si vizuri kwako kwenda pamoja nami mpaka Babuloni, basi, usije. Ujue kwamba waweza kwenda popote katika nchi hii; basi nenda popote unapoamua kuwa pazuri kwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini leo ninakufungua kutoka minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Twende pamoja mpaka Babeli ikiwa unataka, nami nitakutunza, lakini kama hutaki basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda ko kote unakotaka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini leo ninakufungua minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Twende pamoja mpaka Babeli ikiwa unataka, nami nitakutunza. Lakini kama hutaki, basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda kokote unakotaka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya! Leo nazifungua pingu mikononi mwako. Kama unaona ni vema kwenda pamoja nami mpaka Babuloni, basi twende pamoja; mimi nitakutunza vizuri. Lakini kama unaona si vizuri kwako kwenda pamoja nami mpaka Babuloni, basi, usije. Ujue kwamba waweza kwenda popote katika nchi hii; basi nenda popote unapoamua kuwa pazuri kwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa tazama! Nimekufungulia leo minyororo, mikono yako iliyofungwa nayo; vikiwa vema machoni pako kwenda na mimi kufika Babeli, njoo! nitakuangalia kwa macho yangu. Lakini vikiwa vibaya machoni pako kwenda na mimi kufika Babeli, acha! Tazama, nchi hii yote iko mbele yako, patakapokuwa pema kwa kufaa machoni pako, nenda pale!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote i mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, enenda huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi! Leo ninafungua minyororo toka mikono yako. Kama unaona ni vizuri kwenda pamoja nami mpaka Babeli, basi tuende pamoja; mimi nitakutunza vizuri. Lakini kama unaona si vizuri kwako kwenda pamoja nami mpaka Babeli, basi, usikuje. Ujue kwamba unaweza kwenda popote katika inchi hii. Basi kwenda kwenye unaona ni vizuri kwenda.