Jeremiah 40:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ukiamua kubaki, basi rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, ambaye mfalme wa Babuloni amemteua kuwa mtawala wa miji yote ya Yuda, ukakae naye miongoni mwa wananchi wengine. La sivyo, nenda popote unapoona ni sawa kwenda.” Basi, kapteni wa walinzi akampa Yeremia masurufu na zawadi, kisha akamwacha aende zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au uende popote panapokupendeza.” Kisha huyo kiongozi akampa posho yake na zawadi, akamwacha aende zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokuwa bado hajaenda, akasema, Rudi sasa kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa liwali juu ya miji ya Yuda, ukakae pamoja naye kati ya watu; au enenda po pote utakapoona mwenyewe kuwa pakufaa. Basi, amiri wa askari walinzi akampa vyakula na zawadi, akamwacha aende zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ukiamua kubaki, basi rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, ambaye mfalme wa Babuloni amemteua kuwa mtawala wa miji yote ya Yuda, ukakae naye miongoni mwa wananchi wengine. La sivyo, nenda popote unapoona ni sawa kwenda.” Basi, kapteni wa walinzi akampa Yeremia masurufu na zawadi, kisha akamwacha aende zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au nenda po pote panapokupendeza.” Kisha huyo kiongozi akampa mahitaji yake na zawadi na akamwacha aende zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au uende popote panapokupendeza.” Kisha huyo kiongozi akampa posho yake na zawadi, akamwacha aende zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuwa bado hajaenda, akasema, Rudi sasa kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala juu ya miji ya Yuda, ukakae pamoja naye kati ya watu; au nenda popote utakapoona mwenyewe kuwa pakufaa. Basi, mkuu wa askari walinzi akampa vyakula na zawadi, akamwacha aende zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ukiamua kubaki, basi rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, ambaye mfalme wa Babuloni amemteua kuwa mtawala wa miji yote ya Yuda, ukakae naye miongoni mwa wananchi wengine. La sivyo, nenda popote unapoona ni sawa kwenda.” Basi, kapteni wa walinzi akampa Yeremia masurufu na zawadi, kisha akamwacha aende zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokuwa hajaenda bado huko wala huko, akamwambia: Rudi kwake Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Safani, mfalme wa Babeli aliyemweka kuwa msimamizi katika miji ya Yuda, ukae naye katikati yao walio wa ukoo wako! Au po pote palipofaa machoni pako kwenda kukaa, nenda hapo! Kisha mkuu wao waliomlinda mfalme akampa pamba za njiani na matunzo, akampa ruhusa kujiendea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokuwa bado hajaenda, akasema, Rudi sasa kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa liwali juu ya miji ya Yuda, ukakae pamoja naye kati ya watu; au enenda po pote utakapoona mwenyewe kuwa pakufaa. Basi, amiri wa askari walinzi akampa vyakula na zawadi, akamwacha aende zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ukiamua kubaki, basi rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mujukuu wa Safanu, ambaye mufalme wa Babeli amemusimika kuwa mutawala wa miji yote ya Yuda, ukae naye kati ya wanainchi wengine. Kama sivyo, kwenda kwenye unaona unastahili kwenda. Basi, mukubwa wa walinzi akamupa Yeremia vyakula na zawadi, kisha akamwacha ajiendee.