Jeremiah 40:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makapteni wote wa majeshi kutoka bara pamoja na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babuloni alikuwa amemtawaza Gedalia mwana wa Ahikamu, kuwa mkuu wa nchi, na kwamba alikuwa amemkabidhi wanaume, wanawake na watoto, yaani watu mafukara kabisa katika nchi ambao hawakuchukuliwa uhamishoni Babuloni,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi, na amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini zaidi katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa liwali juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makapteni wote wa majeshi kutoka bara pamoja na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babuloni alikuwa amemtawaza Gedalia mwana wa Ahikamu, kuwa mkuu wa nchi, na kwamba alikuwa amemkabidhi wanaume, wanawake na watoto, yaani watu mafukara kabisa katika nchi ambao hawakuchukuliwa uhamishoni Babuloni,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi naye amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini sana katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi, na amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini zaidi katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa mtawala juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makapteni wote wa majeshi kutoka bara pamoja na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babuloni alikuwa amemtawaza Gedalia mwana wa Ahikamu, kuwa mkuu wa nchi, na kwamba alikuwa amemkabidhi wanaume, wanawake na watoto, yaani watu mafukara kabisa katika nchi ambao hawakuchukuliwa uhamishoni Babuloni,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wote wa vikosi waliokuwa bado porini na watu wao waliposikia, ya kuwa mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuisimamia nchi hiyo, akimpa waume na wake na watoto nao wanyonge wa nchi hiyo nao wasiopelekwa Babeli,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa liwali juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wote wa waaskari kutoka katika pori pamoja na watu wao, waliposikia kwamba mufalme wa Babeli alikuwa amemusimika Gedalia mwana wa Ahikamu, kuwa mutawala wa inchi, na kwamba alikuwa amewaweka chini ya usimamizi wake wanaume, wanawake na watoto, ni kusema watu wakosefu kabisa katika inchi ambao hawakupelekwa katika uhamisho kule Babeli,