Jeremiah 41:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Ishmaeli aliwateka binti zake mfalme na watu wote waliosalia Mizpa, watu ambao Nebuzaradani, kapteni wa walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia mwana wa Ahikamu. Ishmaeli mwana wa Nethania, aliwachukua mateka hao, akaondoka, akaenda kwa Waamoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao, yaani, binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Ishmaeli akawachukua mateka watu wote waliosalia, waliokuwa huko Mizpa, yaani, binti za mfalme, na watu wote waliobaki Mizpa, ambao Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia, mwana wa Ahikamu; Ishmaeli, mwana wa Nethania, akawachukua mateka. akaondoka, ili awaendee wana wa Amoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Ishmaeli aliwateka binti zake mfalme na watu wote waliosalia Mizpa, watu ambao Nebuzaradani, kapteni wa walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia mwana wa Ahikamu. Ishmaeli mwana wa Nethania, aliwachukua mateka hao, akaondoka, akaenda kwa Waamoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa kifalme alikuwa amewaacha huko Mizpa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao, ambao ni binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao akavuka kwenda kwa Waamoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao: walikuwa binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Ishmaeli akawachukua mateka watu wote waliosalia, waliokuwa huko Mizpa, yaani, binti za mfalme, na watu wote waliobaki Mizpa, ambao Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia, mwana wa Ahikamu; Ishmaeli, mwana wa Nethania, akawachukua mateka. Akaondoka, ili awaendee wana wa Amoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Ishmaeli aliwateka binti zake mfalme na watu wote waliosalia Mizpa, watu ambao Nebuzaradani, kapteni wa walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia mwana wa Ahikamu. Ishmaeli mwana wa Nethania, aliwachukua mateka hao, akaondoka, akaenda kwa Waamoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Isimaeli akawateka watu wote wa ukoo huu waliosalia Misipa: wana wa kike wa mfalme nao wote pia walioachwa Misipa, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, aliompa Gedalia, mwana wa Ahikamu, awaangalie. Basi, Isimaeli, mwana wa Netania, akawateka, akashika njia kwenda kujitia kwa wana wa Amoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Ishmaeli akawachukua mateka watu wote waliosalia, waliokuwa huko Mizpa, yaani, binti za mfalme, na watu wote waliobaki Mizpa, ambao Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia, mwana wa Ahikamu; Ishmaeli, mwana wa Nethania, akawachukua mateka. akaondoka, ili awaendee wana wa Amoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Isimaeli aliwakamata wabinti wa mufalme mateka na watu wote waliobaki kule Misipa, watu ambao Nebuzaradani, mukubwa wa walinzi, alikuwa amewaweka chini ya ulinzi wa Gedalia mwana wa Ahikamu. Isimaeli mwana wa Netania, aliwakamata mateka hao, akaondoka, akaenda kwa Waamoni.