Jeremiah 41:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Yohanani mwana wa Karea pamoja na viongozi wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, waliwachukua watu wote waliosalia, ambao Ishmaeli mwana wa Nethania, alikuwa amewachukua mateka kutoka Mizpa baada ya kumwua Gedalia mwana wa Ahikamu, yaani: Askari, wanawake, watoto na matowashi. Yohanani aliwarudisha wote kutoka Gibeoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu. Mabaki yao walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yohana, mwana wa Karea, na maakida wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, wakawatwaa hao watu wote waliosalia, aliowapata tena katika mikono ya Ishmaeli, mwana wa Nethania, huko Mizpa, baada ya kumwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, yaani, watu wa vita, na wanawake na watoto, na matowashi, aliowarudisha toka Gibeoni;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Yohanani mwana wa Karea pamoja na viongozi wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, waliwachukua watu wote waliosalia, ambao Ishmaeli mwana wa Nethania, alikuwa amewachukua mateka kutoka Mizpa baada ya kumwua Gedalia mwana wa Ahikamu, yaani: askari, wanawake, watoto na matowashi. Yohanani aliwarudisha wote kutoka Gibeoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika waliotoka Mizpa ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada ya kumwua Gedalia mwana wa Ahikamu, yaani askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu: walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yohana, mwana wa Karea, na viongozi wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, wakawatwaa hao watu wote waliosalia, aliowapata tena katika mikono ya Ishmaeli, mwana wa Nethania, huko Mizpa, baada ya kumwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, yaani, watu wa vita, na wanawake na watoto, na matowashi, aliowarudisha toka Gibeoni;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Yohanani mwana wa Karea pamoja na viongozi wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, waliwachukua watu wote waliosalia, ambao Ishmaeli mwana wa Nethania, alikuwa amewachukua mateka kutoka Mizpa baada ya kumwua Gedalia mwana wa Ahikamu, yaani: Askari, wanawake, watoto na matowashi. Yohanani aliwarudisha wote kutoka Gibeoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa vikosi waliokuwa naye wakawachukua watu wote wa ukoo huu waliosalia, wakawarudisha na kuwatoa kwa Isimaeli, mwana wa Netania, aliowateka Misipa, alipokwisha kumwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, nao walikuwa waume wapigao vita na wanawake na watoto na watumishi wa mfalme wa nyumbani, basi, wakawarudisha toka Gibeoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yohana, mwana wa Karea, na maakida wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, wakawatwaa hao watu wote waliosalia, aliowapata tena katika mikono ya Ishmaeli, mwana wa Nethania, huko Mizpa, baada ya kumwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, yaani, watu wa vita, na wanawake na watoto, na matowashi, aliowarudisha toka Gibeoni;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Yohana mwana wa Karea pamoja na wakubwa wote wa waaskari waliokuwa pamoja naye, waliwakamata watu wote waliobaki, ambao Isimaeli mwana wa Netania, alikuwa amewakamata mateka kutoka Misipa kisha kumwua Gedalia mwana wa Ahikamu, ni kusema: waaskari, wanawake, watoto na matowashi wa nyumba ya mufalme. Yohana aliwarudisha wote kutoka Gibeoni.