Jeremiah 41:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi, wakainuka na kumshambulia kwa upanga Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, wakamuua. Gedalia ndiye aliyekuwa ameteuliwa na mfalme wa Babuloni kuwa mtawala wa nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga; wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaondoka huyo Ishmaeli, mwana wa Nethania, na watu wale kumi waliokuwa pamoja naye, wakampiga Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, kwa upanga, wakamwua; yeye ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa liwali wa nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi, wakainuka na kumshambulia kwa upanga Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, wakamuua. Gedalia ndiye aliyekuwa ameteuliwa na mfalme wa Babuloni kuwa mtawala wa nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumwua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani kwa upanga, wakamwua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemweka awe mtawala juu ya nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga, wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaondoka huyo Ishmaeli, mwana wa Nethania, na watu wale kumi waliokuwa pamoja naye, wakampiga Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, kwa upanga, wakamwua; yeye ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala wa nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi, wakainuka na kumshambulia kwa upanga Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, wakamuua. Gedalia ndiye aliyekuwa ameteuliwa na mfalme wa Babuloni kuwa mtawala wa nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Isimaeli, mwana wa Netania, alipoinuka na wale watu kumi waliokuwa naye, wakampiga Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Safani, kwa panga, mpaka wakamwua; naye ndiye, mfalme wa Babeli aliyemweka kuisimamia nchi hiyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaondoka huyo Ishmaeli, mwana wa Nethania, na watu wale kumi waliokuwa pamoja naye, wakampiga Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, kwa upanga, wakamwua; yeye ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa liwali wa nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isimaeli mwana wa Netania pamoja na wale watu kumi, wakasimama na kumushambulia kwa upanga Gedalia mwana wa Ahikamu, mujukuu wa Safanu, wakamwua. Gedalia ndiye aliyekuwa amesimikwa na mufalme wa Babeli kuwa mutawala wa inchi.