Jeremiah 41:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kabla hata mtu yeyote hajajua habari hizo, walifika watu themanini kutoka Shekemu, Shilo na Samaria. Walikuwa wamenyoa ndevu zao na wamevaa mavazi yaliyotatuka na miili yao imechanjwachanjwa. Walileta tambiko za nafaka na ubani zitolewe hekaluni kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakafika watu kadha wa kadha toka Shekemu, na toka Shilo, na toka Samaria, watu themanini, nao wamenyoa ndevu zao, na kurarua nguo zao, nao wamejikata-kata, wakichukua sadaka na ubani mikononi mwao, ili wazilete nyumbani kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kabla hata mtu yeyote hajajua habari hizo, walifika watu themanini kutoka Shekemu, Shilo na Samaria. Walikuwa wamenyoa ndevu zao na wamevaa mavazi yaliyotatuka na miili yao imechanjwachanjwa. Walileta tambiko za nafaka na ubani zitolewe hekaluni kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakafika watu kadhaa toka Shekemu, na toka Shilo, na toka Samaria, watu themanini, nao wamenyoa ndevu zao, na kurarua nguo zao, nao wamejikatakata, wakichukua sadaka na ubani mikononi mwao, ili wazilete nyumbani kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kabla hata mtu yeyote hajajua habari hizo, walifika watu themanini kutoka Shekemu, Shilo na Samaria. Walikuwa wamenyoa ndevu zao na wamevaa mavazi yaliyotatuka na miili yao imechanjwachanjwa. Walileta tambiko za nafaka na ubani zitolewe hekaluni kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaja watu waliotoka Sikemu na Silo na Samaria, nao walikuwa watu 80 waliojinyoa ndevu na kuvaa nguo zilizoraruliwa, tena walikuwa wamejikatakata chale, namo mikononi mwao walichukua vipaji vya tambiko na uvumba kuvipeleka Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakafika watu kadha wa kadha toka Shekemu, na toka Shilo, na toka Samaria, watu themanini, nao wamenyoa ndevu zao, na kurarua nguo zao, nao wamejikata-kata, wakichukua sadaka na ubani mikononi mwao, ili wazilete nyumbani kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mbele hata mutu yeyote hajajua habari hizo, kulifika watu makumi nane kutoka Sekemu, Shilo na Samaria. Walikuwa wamenyoa ndevu zao na wamevaa nguo zilizotatuka na miili yao imechanjwachanjwa. Walileta sadaka ya ngano na ubani vitolewe katika nyumba ya Yawe.