Jeremiah 41:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini palikuwa na watu kumi katika kundi hilo waliomwambia Ishmaeli: “Tafadhali usituue, maana tuna akiba kubwa ya ngano, shayiri, mafuta na asali ambayo tumeificha mashambani.” Basi hao akawaacha hai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watu kumi walionekana miongoni mwao, waliomwambia Ishmaeli, Usituue; kwa maana tuna akiba zetu zilizofichwa kondeni, za ngano, na shayiri, na mafuta, na asali. Basi, akawaacha, asiwaue watu hao pamoja na ndugu zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini palikuwa na watu kumi katika kundi hilo waliomwambia Ishmaeli: “Tafadhali usituue, maana tuna akiba kubwa ya ngano, shayiri, mafuta na asali ambayo tumeificha mashambani.” Basi hao akawaacha hai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watu kumi walionekana miongoni mwao, waliomwambia Ishmaeli, Usituue; kwa maana tuna akiba zetu zilizofichwa shambani, za ngano, na shayiri, na mafuta, na asali. Basi, akawaacha, asiwaue watu hao pamoja na ndugu zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini palikuwa na watu kumi katika kundi hilo waliomwambia Ishmaeli: “Tafadhali usituue, maana tuna akiba kubwa ya ngano, shayiri, mafuta na asali ambayo tumeificha mashambani.” Basi hao akawaacha hai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao wale kukaonekana watu kumi, wakamwambia Isimaeli: Usituue! Kwani tuko na vilimbiko, tulivyovificha porini, vya ngano na vya mawele na vya mafuta na vya asali; ndipo, alipowaacha, asiwaue pamoja na ndugu zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watu kumi walionekana miongoni mwao, waliomwambia Ishmaeli, Usituue; kwa maana tuna akiba zetu zilizofichwa kondeni, za ngano, na shayiri, na mafuta, na asali. Basi, akawaacha, asiwaue watu hao pamoja na ndugu zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kulikuwa watu kumi katika kundi hilo waliomwambia Isimaeli hivi: Tafazali usituue, maana tuna akiba kubwa ya ngano, shayiri, mafuta na asali ambayo tumeificha katika pori. Basi hao akawaacha wazima.