Jeremiah 41:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisima ambamo Ishmaeli alitupa maiti za wale watu aliowaua kilikuwa ni kile kikubwa, ambacho mfalme Asa alikuwa amekichimba ili kujihami dhidi ya Baasha, mfalme wa Waisraeli. Ishmaeli mwana wa Nethania, alikijaza kisima hicho maiti za wale watu aliowaua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya kuwa sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, shimo lile, ambalo Ishmaeli ameitupa mizoga ya watu aliowaua, karibu na Gedalia, (ni lile lile alilolichimba Asa, mfalme, kwa kuwa alimwogopa Baasha, mfalme wa Israeli), Ishmaeli, mwana wa Nethania, akalijaza kwa watu wale aliowaua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisima ambamo Ishmaeli alitupa maiti za wale watu aliowaua kilikuwa ni kile kikubwa, ambacho mfalme Asa alikuwa amekichimba ili kujihami dhidi ya Baasha, mfalme wa Waisraeli. Ishmaeli mwana wa Nethania, alikijaza kisima hicho maiti za wale watu aliowaua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, shimo lile, ambalo Ishmaeli amezitupa maiti za watu aliowaua, karibu na Gedalia, (ni lile lile alilolichimba Asa, mfalme, kwa kuwa alimwogopa Baasha, mfalme wa Israeli), Ishmaeli, mwana wa Nethania, akalijaza kwa watu wale aliowaua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisima ambamo Ishmaeli alitupa maiti za wale watu aliowaua kilikuwa ni kile kikubwa, ambacho mfalme Asa alikuwa amekichimba ili kujihami dhidi ya Baasha, mfalme wa Waisraeli. Ishmaeli mwana wa Nethania, alikijaza kisima hicho maiti za wale watu aliowaua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hicho kisima, Isimaeli alimoitumbukizia mizoga yao yote, aliowaua, walipokuja kwa Gedalia, ni kile, mfalme Asa alichokifanya kwa ajili ya kupigana na Basa, mfalme wa Isiraeli; hicho ndicho, Isimaeli, mwana wa Netania, alichokijaza mizoga yao, aliowaua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, shimo lile, ambalo Ishmaeli ameitupa mizoga ya watu aliowaua, karibu na Gedalia, (ni lile lile alilolichimba Asa, mfalme, kwa kuwa alimwogopa Baasha, mfalme wa Israeli), Ishmaeli, mwana wa Nethania, akalijaza kwa watu wale aliowaua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisima ambamo Isimaeli alitupa maiti za wale watu aliowaua ni kile kikubwa ambacho mufalme Asa alikuwa amekichimba kwa kujikinga na Basha, mufalme wa Waisraeli. Isimaeli mwana wa Netania alikijaza kisima hicho maiti za wale watu aliowaua.