Jeremiah 42:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho Mwenyezi Mungu, wala sitawaficha chochote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba Bwana, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lo lote ambalo Bwana atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba BWANA Mungu wenu kama mlivyoomba, nitawaambia kila kitu asemacho BWANA wala sitawaficha cho chote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba bwana Mwenyezi Mungu wenu kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho bwana, wala sitawaficha chochote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba BWANA, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lolote ambalo BWANA atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfumbuaji Yeremia akawaambia: Nimesikia; sasa hivi nitawaombea kwa Bwana Mungu wenu kwa ajili ya njia yenu; kila neno, Bwana atakalowajibu, nitawaambia, sitawanyima neno kamwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba BWANA, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lo lote ambalo BWANA atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeremia akawajibu: Vema; nimesikia. Nitamwomba Yawe, Mungu wenu, kama mulivyonisihi; jibu lolote Yawe atakalonipa, nitawaambia; sitawaficha kitu chochote.