Jeremiah 42:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Iwe ni jambo la kupendeza au la, sisi tutaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu ambaye tunakutuma kwake ili tufanikiwe tutakapomtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Iwe ni jambo la kupendeza au la, sisi tutaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu ambaye tunakutuma kwake ili tufanikiwe tutakapomtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii BWANA Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii BWANA Mungu wetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii bwana Mwenyezi Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii bwana Mwenyezi Mungu wetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Iwe ni jambo la kupendeza au la, sisi tutaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu ambaye tunakutuma kwake ili tufanikiwe tutakapomtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ni jema au kama ni baya, sauti ya Bwana Mungu wetu tutaisikia, kwa kuwa tunakutuma kwake, kusudi tuone mema tukiisikia sauti ya Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikuwe ni jambo la kupendeza au hapana, sisi tutaitii sauti ya Yawe, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake kusudi mambo yatuendekee vizuri tutakapomutii Yawe, Mungu wetu.