Jeremiah 43:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha utawala juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema lake la ufalme juu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukawaambie, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitatuma na kumtwaa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitaweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya niliyoyaficha; naye atatandaza hema yake ya fahari juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza chandarua yake ya kifalme juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema yake ya ufalme juu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukawaambie, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitatuma na kumtwaa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitaweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya niliyoyaficha; naye atatandaza hema yake ya fahari juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Mtaniona, ninavyomtuma na kumchukua mtumishi wangu Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, nikiweka kiti chake cha kifalme juu ya mawe haya, niliyoyafukia, naye ataliwamba hema lake lenye utukufu juu yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukawaambie, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitatuma na kumtwaa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitaweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya niliyoyaficha; naye atatandaza hema yake ya fahari juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha uwaambie hivi: Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Muangalie, mimi nitamutuma na kumuleta Nebukadneza, mufalme wa Babeli, mutumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha kifalme juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.