Jeremiah 43:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri; naye Nebukadneza ataiteketeza miungu hiyo kwa moto au kuichukua mateka mpaka Babuloni. Ataisafisha nchi ya Misri kama mchungaji atoavyo kupe katika vazi lake na kuondoka Misri akiwa mshindi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atachoma moto mahekalu ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama mchungaji ajizungushiavyo vazi lake, ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo kwa amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawasha moto katika nyumba za miungu ya Misri, na kuziteketeza, na kuwachukua mateka; naye atajipamba kwa nchi ya Misri, kama vile mchungaji avaavyo nguo zake; naye atatoka huko na amani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri; naye Nebukadneza ataiteketeza miungu hiyo kwa moto au kuichukua mateka mpaka Babuloni. Ataisafisha nchi ya Misri kama mchungaji atoavyo kupe katika vazi lake na kuondoka Misri akiwa mshindi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atachoma moto mahekalu yao ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama vile mchungaji ajizungushiavyo vazi lake ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo bila kudhurika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atachoma moto mahekalu yao ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama vile mchungaji ajizungushiavyo vazi lake ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo bila kudhurika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawasha moto katika nyumba za miungu ya Misri, na kuziteketeza, na kuwachukua mateka; naye atajipamba kwa nchi ya Misri, kama vile mchungaji avaavyo nguo zake; naye atatoka huko na amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri; naye Nebukadneza ataiteketeza miungu hiyo kwa moto au kuichukua mateka mpaka Babuloni. Ataisafisha nchi ya Misri kama mchungaji atoavyo kupe katika vazi lake na kuondoka Misri akiwa mshindi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo katika nyumba za miungu ya Misri nitatia moto, naye ataziteketeza, nayo miungu ataiteka; atajivika nchi ya Misri, kama mchungaj anavyojivika nguo yake, kisha atatoka huku na kutengemana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawasha moto katika nyumba za miungu ya Misri, na kuziteketeza, na kuwachukua mateka; naye atajipamba kwa nchi ya Misri, kama vile mchungaji avaavyo nguo zake; naye atatoka huko na amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri; naye Nebukadneza ataiteketeza miungu hiyo kwa moto au kuikamata mateka mpaka Babeli. Ataisafisha inchi ya Misri kama muchungaji anavyoondoa vidudu katika nguo yake na kuondoka Misri akiwa mushindi.